RAIS WA KOREA KASKAZINI KIM-JONG-UN


                            HISTORIA FUPI YA RAIS WA KOREA KASKAZINI KIM-JONG-UN
MJUE KIM JONG-UN
Kim Jong- un ni mtoto wa tano na wa mwisho ktk uzao wa Kim jog-il( raisi wa pili wa Korea Kaskazini) na kwa sasa ndo kiongozi wa nchi hiyo na alichukua cheo hicho baada ya kifo cha baba yake Dec 19, 2011.
Kim jong-un anatajwa kuwa mmoja wa viongozi wenye msimamo mkali hasa kwa nchi za kimagharibi na hadi sasa anaimarisha nguvu za kinyuklia za korea kaskazini na anainyima usingizi marekan....Tuyajue machache yafuatayo kuhusu Kim jong-un
1 Ni general pekee duniani aliyepata cheo hicho bila uzoefu wa kijeshi.Kipaji,akili na kujituma ndo vilimfanya kuwa general licha ya kutokuwa na mafunzo wala uzoefu wowote wa masuala ya kijeshi.Labda ni kwa sbb Kim ni shupavu na jasiri wa kuzaliwa na sio wa kujifunza.Ana nyota nne begani na anapenda zana za kinyuklia kuliko zana nyingne za kijeshi
2 Pamoja na kuwa kiongozi na mkuu wa nchi, Kim hakusoma shule yoyote nchini korea kaskazini.Alipelekwa kwa siri nchini Swirtzerland akiwa mdogo na alisoma Bern international school nchini humo. Mkuu wa shule alimtambulisha darasa la sita A kama Park un na kwamba alkuwa mtoto wa mwanadiplomasia wa korea kaskazini (kwa sbb za kiusalama).Somo alilofaulu vizuri ni mziki lkn alifeli hesabu na sayansi.
3 Anaweza kuwa ndo kiongozi mkubwa wa nchi na mwenye umri mdogo zaidi dunian japo haifahamiki ni lini hasa Kim jong-un alizaliwa. Wapo wanaodai alizaliwa mwaka 1982, wengne 1983, na taarfa nyingne zinasema alzaliwa mwaka 1984.
4 Baba yake, Kim jong-il alizaliwa kimiujiza. Taarifa nchini korea kaskazin zinasema Kim jong-il alizaliwa mlima Baekdu. Huu ni mlima wa imani na huabudiwa na wakorea kaskazin. Wakati,saa na siku aliyozaliwa, nyota mpya ilitokea na kufunika mbingu, ghafla majira yalibadilka kutoka winter kwenda spring na pinde mbili za mvua zilionekana. Japo taarifa kutoka ktk kumbukumbu za kisoviet zinasema jamaa alizaliwa 1941 ktk kijiji cha Vyatskoye huko nchini siberia. Huyu ni baba wa kim jong-un.
5 Taarifa nyingne weird ni kwamba baba yake na kim jong-un yaan hayati kim jong-il hakuwahi kwenda haja kubwa wala haja ndogo maisha yake yote na alikuwa na uwezo wa kubadili majira na hali ya hewa.
6 Akiwa na miaka 27 Kim jong-un alifanyiwa plastic surgery ili kuwa na mwonekano sawa na babu yake Kim II sung. Hii ni kwa sbb wakorea kaskazin wengi hawamiliki vyombo vya habari na hivywengi hawakuwahi kumuona ila siku walipomuona walimfananisha na hayati kim II sung na kwa hilo wakatokea kumpenda sana kwakuwa alifanana na babu yake ambaye ndo baba wa taifa wa korea kaskazin na kwao huyu ni Mungu wao na wanaamini yupo nao hadi leo ktk maisha yake ya nje ya uhai.
7 Mwaka 2012, wachina walidai Kim jong-un ni "Sexiet man alive " na kwamba jamaa ni ndoto ya kila mwanamke hapa duniani. Hii ni kutokana na mwonekano wake,ushupavu,ukarimu, kujiamini as well as round and handsome face yake....ha ha haaaaa!
8 Baba yake alipofariki mwaka 2011 alihakikisha msiba wake unaombolezwa na wakorea kaskazin wote. Ambao hawakujua namna ya kulia machozi ya mamba alihakikisha wanayatoa. Ambao hawakushiriki kwa namna moja ama nyingne ktk shughuli muhimu za msiba huo yakiwemo mazishi walihukumiwa kufanya kazi ngumu miezi sita.
9 Alimuhukum kifo kamanda msaidizi wa jeshi la wananchi kwa kosa la kuhudhuria msiba wa baba yake akiwa amelewa. Amri aliyoitoa ni kwamba " anyongwe na usibaki hata unywele wake". Huyo ndo kim jong-un
10 Kim jong-un pia alitoa hukumu ya kifo kwa mjomba wake kwa kile kinachodaiwa kuwa kosa la ubadhilifu wa mali ya umma na harakati za kupindua nchi. Huyu alivuliwa nguo na kutupwa ktk banda la mbwa wakali waliomzika ktk matumbo yao.
11 Mtindo wake wa unyoaji nywele ni maarufu sana ndani na nje ya korea kaskazini. Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini humo wameshauriwa kuiga mtindo huo wa unyoaji nywele wa rais wao.
12 Kim jong-un hujinyoa nywele zake yeye mwenyewe na hana kinyozi yeyote kwa kile anachokiita sbb za kiusalama na anasema hawaamini vivyozi.
13 Mmoja kati ya marafiki wakuba wa kim jong-un ni nyota wa zaman wa NBA Michael Jordan. Akiwa mwanafunzi, kim alitumia muda wake mwingi kuchora picha za Michael Jordan.
Huyo ndo KIM JONG-UN kamanda anayewanyima amani korea kusini na mshirika wake Marekani na anadai yupo tayari kwa lolote dhidi ya marekani hasa kwa nguvu za kinyuklia. Anaendeleza kile walichokiamini babu na baba yake kuwa Marekan ndo adui mkubwa wa korea kaskazin.

Comments

Popular posts from this blog

KOREA KASKAZINI YAFUTA MKUTANO WAKE NA KOREA KUSINI GHAFLA JUU YA MAZOEZI YA MALEKANI