KOREA KASKAZINI YAFUTA MKUTANO WAKE NA KOREA KUSINI GHAFLA JUU YA MAZOEZI YA MALEKANI
Sambaza habari hii Facebo Sambaza habari hii Twitter Sambaza habari hii Messenger Sambaza Korea ya Kaskazini imesitisha mazungumzo yaliyotarajiwa kufanyika mapema wiki hii dhidi ya Korea ya Kusini kwa sababu ya kuchukizwa kwake na mazoezi ya kijeshi ya pamoja na Marekani. Maafisa wa shirika la habari la Korea ya Kaskazini KCNA wameeleza kuwa mazoezi hayo ni sehemu ya mazoezi ya "chuki" na kuyachukulia kama mazoezi ya uvamizi. Lakini pia kuna onyo lililotolewa na Marekani juu ya hatima ya mkutano wa kihistoria kati ya Kim Jong-un na Rais wa Marekani Donald Trump ambao umepangwa tarehe 12 Juni. Kim Jong-un atishia kufuta mkutano wake na Trump Ikumbukwe kwamba katika ya mwezi wa tatu mwaka huu, Mr Trump aliushangaza ulimwengu kwa kukubali mwaliko wa kukutana na rasi Kim, na kujinasibu kuwa "Tutajaribu kuufanya mkutano wetu kuwa wa wakati wa pekee wa Amani ya Dunia!" raisi wa Marekani aliandika haya kwenye mtandao wa Twitter wakati huo ka...