Posts

Showing posts from May 21, 2018

KUMBUKUMBU YA KUZAMA KWA MELI YA MV BUKOBA MEI 21.1996

Image
Meli ya Mv Bukoba Ikiwa Ziwa Victoria Wakati Ilipokuwa ikitoa huduma ya usafirishaji kabla ya kuzama. Kiukweli Tarehe kama ya leo miaka 21 iliyopita haitoweza kusahaulika kirahisi kwenye mioyo ya watanzania na ulimwengu kote. kwani usiku wa kuamkia mei 21. 1996. Meli ya Mv Victoria ikiwa na abiria kati ya 750 na 800 pamoja na wafanyakazi 37 ilizama majini kwenye ziwa victoria mwambao wa bwiru jijini mwanza ambapo ilikuwa takribani kilomita 30 kufika nchi kavu Meli ya Mv bukoba ikiwa inazama. Ripoti ya Tume ya Jaji Robert Kisanga, iliyochunguza chanzo cha hiyo ilieleza kuwa, kati ya hao, 114 waliokolewa wakiwa hai; wakati 391 waliopolewa wakiwa wamefariki na kuzikwa katika makaburi ya Igoma barabara ya Musoma, nje kidogo ya Jiji la Mwanza. Miili mingine ilichukuliwa na jamaa kuzikwa kwao. Jumla ya miili 332 haikupatikana. Kila mwaka, ifikapo Mei 21, viongozi wa dini, wa serikali na wananchi huongozana kwenda eneo la ajali kufanya kumbukumbu.   Kumbukumbu ya Kuza...